Skip to main content

Faragha katika Microsoft

Data yako, uzoefu wako wa uendeshaji, unaudhibiti.

Katika Microsoft, lengo letu ni kuwezesha kila mtu na kila shirika ulimwenguni kufanikiwa zaidi. Tunafanya haya kwa kujenga wingu bora zaidi, kubuni upya uzalishaji na michakato ya biashara na kubinafsisha zaidi ukokotoaji. Katika shughuli hizi zote, tunaimarisha thamani ya faragha isiyo na kipimo na uwezo wako wa kudhibiti data yako.

Hii huanza kwa kuhakikisha kuwa unapata chaguo muhimu kuhusu jinsi na mbona data inakusanywa na kutumiwa, na kuhakikisha kuwa una maelezo unayohitaji ili kufanya maamuzi ambayo ni sahihi kwako kuhusu bidhaa na huduma zetu.

Tunajitahidi kukuza imani yako kila siku kwa kulenga kanuni sita kuu za faragha:

  • Udhibiti: Tutakufanya udhibiti faragha yako kwa zana ambazo ni rahisi kutumia na chaguo wazi.
  • Uwazi: Tutakuwa wazi kuhusu ukusanyaji na matumizi ya data yako ili uweze kufanya maamuzi ya busara.
  • Usalama: Tutalinda data unayotupa kupitia usalama na usimbaji fiche thabiti.
  • Ulinzi thabiti wa kisheria: Tutaheshimu sheria zako za faragha ya ndani na kupigania ulinzi halali wa faragha yako kama haki msingi ya binadamu.
  • Hakuna ulengaji unaotegemea muktadha: Hatutatumia barua pepe, sogoa, faili au maudhui yako mengine ya kibinafsi kulenga matangazo kwako.
  • Manufaa yako: Tunapokusanya data, tutaitumia kukunufaisha na kuboresha uzoefu wako.

Kanuni hizi zinaunda msingi wa mfumo wa faragha ya Microsoft na utaendelea kuandaa jinsi tunavyoimarisha bidhaa na huduma zetu. Kwa wateja wa kampuni kubwa na biashara, angalia Kituo cha Uaminifu cha Microsoft ili kujifunza jinsi ya kulinda data yako katika Wingu la Microsoft.

Katika sehemu nyinginezo za tovuti hii, utapata viungo vitakavyokupatia maelezo zaidi pamoja na udhibiti ili kukuruhusu kufanya maamuzi bora kwa ajili yako mwenyewe. Na tunaendelea kujitahidi kuimarika, kwa hivyo iwapo utagundua kitu chochote katika bidhaa na huduma zetu ambacho hakifanyiki jinsi ulivyotarajia kuhusu faragha, tafadhali tufahamishe.


Je, Microsoft inakusanya aina zipi za data?

Microsoft hukusanya data ili kukusaidia kufanya mambo zaidi. Ili kufanya hivi, tunatumia data tunayokusanya kuendesha na kuboresha programu, huduma, na vifaa vyetu, kukupa uzoefu uliobinafsishwa na kusaidia kukulinda. Hizi ni baadhi ya kategoria za kawaida zaidi za data tunayokusanya.

Kuvinjari kwenye wavuti na utafutaji wa mtandaoni

Mwanamke anavinjari wavuti na kufanya utafutaji

Kama tu injini nyingi za utafutaji, tunatumia historia yako ya utafutaji, na historia iliyojumlishwa kutoka kwa watu wengine, ili kukupatia matokeo bora ya utafutaji. Ili kuongeza kazi ya kuvinjari kwa wavuti, vivinjari vya wavuti vya Microsoft vinaweza kukusanya na kutumia historia ya kuvinjari ili kubashiri unapotaka kuenda. Cortana inaweza kutoa mapendekezo yaliyobinafsishwa kulingana na kuvinjari kwako na historia ya utafutaji.

Unaweza kuchagua iwapo historia yako ya kuvinjari inakusanywa kupitia Majibu na Mipangilio ya Kikagua Matatizo katika mipangilio yako ya faragha ya Windows. Kadhalika, unaweza kudhibiti iwapo Cortana inafikia utafutaji na historia yako ya kuvinjari katika mipangilio ya Cortana na Microsoft Edge.

Maeneo unayoenda

Kuendesha gari karibu na duka la aiskrimu

Maelezo ya eneo hutusaidia kutoa maelekezo katika maeneo unayotaka kuenda na kukuonyesha maelezo muhimu mahali ulipo. Kwa hili, tunatumia maeneo unayotoa au yale tuliyotambua kutumia teknolojia kama anwani za GPS au IP.

Kutambua eneo pia hutusaidia kukulinda. Kwa mfano, iwapo karibu kila mara unaingia ukiwa Tokyo, na ghafla unaingia ukiwa London, tunaweza kuangalia ili kuhakikisha kwa kweli ni wewe.

Unaweza kuwasha au kuzima huduma za eneo kwa kifaa chako katika Mipangilio > Faragha> Eneo. Kutoka hapa, pia unaweza kuchagua programu zipi za Microsoft Store zina ufikiaji katika eneo lako na kudhibiti historia ya eneo iliyohifadhiwa kwenye kifaa chako.

Ili kutazama na kufuta data ya eneo ambayo imehusishwa na akaunti yako ya Microsoft, nenda kwenye account.microsoft.com.

Data inayotuwezesha kukusaidia, kibinafsi

Mwanamume anaangalia simu akaiwa kwenye njia ya wapitao kwa miguu

Ili kukusaidia kuepuka trafiki, kumbuka maadhimisho, tumia matini sahihi “Jennifer” kwenye orodha yako ya mwasiliani, na kwa jumla fanya zaidi, Cortana inahitaji kujua kinachokupendeza, kile kilicho kwenye kalenda yako, na nani unayeweza kutaka kufanya mambo naye. Wakati hutaki kutumia kibodi, tunaweza kutumia usemi na ruwaza ya muandiko wako ili kusaidia kutafsiri kile unachosema au kuandika katika nyaraka na ujumbe wa matini.

Dhibiti mapendeleo yako ya Cortana na data nyingine

Mazoezi ya mwili na afya

Mwanamume anaendesha baiskeli mtaani

Microsoft Health, HealthVault na vifaa kama Microsoft Band vinaweza kukusaidia kuelewa na kudhibiti data yako ya afya.

Data yako inaweza kujumuisha data ya muda halisi kama mpigo wako wa moyo na hatua unazotembea kila siku. Pia inaweza kujumuisha rekodi zako za afya iwapo utachagua kutumia HealthVault kuhifadhi data hiyo. HealthVault pia hukuwezesha kushiriki rekodi za afya na mtoa huduma wako.

Data tunayotumia kuonyesha matangazo zaidi ya kuvutia

Mwanamke anatembea barabara ya chini ya mtaa

Baadhi ya huduma za Microsoft zinaauniwa kwa utangazaji. Ili kuonyesha matangazo ambayo una uwezekano wa kupendezwa nayo, tunatumia data kama eneo lako, utafutaji wa wavuti wa Bing, kurasa za Microsoft au kurasa za wavuti wa mtangazaji unazotazama, demografia, na mambo uliyopendelea. Hatutumii kile unachosema kwenye barua pepe, sogoa, simu za video au barua ya sauti, au nyaraka zako, picha au faili nyingine za kibinafsi ili kulenga matangazo kwako.

Ili kusitisha Microsoft kukuonyesha matangazo kuzingatia mapendeleo yako, tumia vidhibiti vyetu vya utangazaji mtandaoni. Bado utaona matangazo, lakini huenda yasikupendeze.

Data ya kuingia na malipo

Mwanamume analipia kahawa

Kusajili akaunti yako binafsi ya Microsoft hukuwezesha kutumia huduma za mtandaoni kama mipangilio ya hifadhi na familia, na husaidia kuiweka mipangilio yako kulandana na vifaa vinginevyo vinavyotumika. Unapoongeza data ya malipo kwenye akaunti yako, kupata programu, kujisajili, kupata filamu, televisheni, na michezo huwa rahisi kwenye vifaa vyako vya Windows 10.

Kwa kuweka nywila yako kwa usiri, na kuongeza maelezo ya ziada ya usalama kama nambari ya simu au anwani ya barua pepe, unaweza kusaidia kuhifadhi faili, kadi za mkopo, historia ya kuvinjari, na maelezo yako ya eneo salama kabisa.

Ili kusasisha nywila, maelezo ya usalama, na chaguo za malipo, tembelea Tovuti ya akaunti ya Microsoft.

Maelezo kutoka kwenye vihisio vya kifaa

Mwanamume anaketi kwenye kochi akiwa na vifaa vilivyounganishwa

Jinsi ungetarajia kutoka kwa kifaa chochote cha kisasa, simu za Windows 10, kompyuta ndogo, na kompyuta zaidi huja na vihisio—njia za vifaa kutambua ulimwengu. Hiyo inaweza kuwa maikrofoni au akseleromita ya simu yako, kitambazaji cha alama ya vidole cha kompyuta yako ya mkononi, na kihisio cha ndani cha GPS, na zaidi.

Katika vifaa vya Windows 10, unadhibiti data ipi ya kihisio kifaa na programu zinaweza kutumia kwenye Mipangilio > Faragha.


Windows 10 na huduma zako za mtandaoni

Nembo ya Windows 10
Mwanamke anatumia kompyuta ya mkononi kwenye dawati

Ukiwa na Windows 10 kama huduma inayowezeshwa kwa wingu, data hutusaidia kuendelea kulinda na kuboresha tajiriba yako. Kwa mfano, ili kusaidia kukulinda mtandaoni, tunatambaza kiotomatiki vifaa vya Windows 10 kwa programu hasidi zinazojulikana. Kadhalika, tunatumia telemetri, ambayo ni maelezo yanayoendelea tunayopokea kuhusu jinsi mfumo wako wa Windows 10 unavyoendeshwa, ili kufanya kifaa chako kuendeshwa vizuri. Kwa hivyo iwapo tunajua kuna tatizo kwa aina fulani ya kiendeshi cha kichapishaji, tunaweza kutuma viendeshi sahihi kwa watu wanaotumia aina hiyo ya kichapishaji tu.

Kadhalika, tunakupa idadi ya vidhibiti vya jinsi maelezo yanavyotumika kuwasilisha huduma zilizobinafsishwa na uzoefu kwenye Windows 10. Unaweza kurekebisha mipangilio yako ya faragha ya Windows 10 kwa kila kitu kutoka kwenye telemetri msingi hadi huduma zilizobinafsishwa wakati wowote kwa kuenda kwenye Mipangilio > Faragha > Majibu na uchunguzi.

Jifunze jinsi kila bidhaa zetu hutumia data ili kubinafsisha uzoefu wako.

Office Nembo ya Office

Tazama mipangilio ya faragha kwenye programu yoyote ya Office kwa kuenda kwenye Faili > Chaguo > Kituo cha Uaminifu.

Mipangilio katika Kituo cha Uaminifu

Skype Nembo ya Skype

Hariri anayeweza kuona wasifu wako kwenye Skype na mipangilio mingine ya faragha katika Skype.com.

Mipangilio ya Skype

OneDrive Nembo ya OneDrive

Unadhibiti anayeweza kutazama faili zako kwenye OneDrive.

Shughuli bora za kulinda faili zako

Xbox Nembo ya Xbox

Rekebisha mipangilio yako ya faragha ya Xbox kwenye kiweko chako au Xbox.com.

Mipangilio ya faragha ya Xbox

Bing Nembo ya Bing

Zima Mapendekezo ya Utafutaji na urekebishe mipangilio mingine kwa kuingia kwenye Bing.com.

Mipangilio ya faragha ya Bing

Cortana Nembo ya Cortana

Cortana hufanya kazi bora zaidi inapokufahamu kutoka kwenye kifaa chako na huduma nyingine za Microsoft.

Mipangilio ya Cortana